1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Leverkusen kuvaana na Stuttgart kuwania Kombe la Supercup

12 Agosti 2024

Mabingwa wa ligi kuu ya soka Ujerumani, Bundesliga, Bayer Leverkusen watachuana na VfB Stuttgart iliyomaliza katika nafasi ya pili msimu uliopita kuwania ubingwa wa Kombe la Supercup Agosti 17 katika uwanja wa Bay Arena.

https://p.dw.com/p/4jOIt
Fußballspieler Granit Xhaka
Wachezaji wa Bayer Leverkusen wakisherehekea ushindi baada ya kuifunga Kaiserslautern 1-0 katika fainali ya Kombe la shirikisho la Ujerumani DFP-PokalPicha: Frank Hoermann/SVEN SIMON/picture alliance

Tangu jadi, mechi ya kufungua pazia ya msimu mpya huwakutanisha mabingwa wa Bundesliga na mshindi wa Kombe la Shirikisho la Ujerumani DFB Pokal.

Hata hivyo, baada ya Bayer Leverkusen kushinda mataji yote mawili, VfB Stuttgart iliyomaliza katika nafasi ya pili imepata fursa ya kumenyana na vijana wa Xabi Alonso.

Mechi ya Kombe la Supercup itachezwa Jumamosi hii ya Agosti 17 katika dimba la Bay Arena.

Wakati huo huo, mshambuliaji wa klabu ya Hoffenheim Maximilian Beier amejiunga na Borussia Dortmund.

Soma pia: Dani Olmo ajiunga na Barcelona akitokea Leipzig

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21, aliyecheza mechi moja pekee wakati wa michuano ya kombe la mataifa ya Ulaya EURO 2024, atasaini mkataba wa miaka mitano kuichezea Dortmund.

Dortmund, iliyomaliza katika nafasi ya tano msimu uliopita, inatarajiwa kulipa euro milioni 30 kama ada ya uhamisho. Beier atachukua nafasi ya Niclas Füllkrug aliyejiunga na wananyundo nchini Uingereza Westham United.

Hadi sasa, Borussia Dortmund imewasaini Serhou Guirassy na Waldermar Anton wakitokea VfB Stuttgart, Pascal Gross kutoka Brighton na Yan Couto wa Manchester City.

Ujio wa Maximilian Beier ndani ya Signal Iduna Park kunafungua njia kwa mshambuliaji kinda Youssoufa Moukoko kuondoka klabuni humo.