1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Leo ni mwanzo wa mwezi wa Ramadhani kwa Waislamu wengi

11 Machi 2024

Saudi Arabia, Qatar na Umoja wa Falme za Kiarabu zilitangaza mwezi mtukufu wa Ramadhan, katika kipindi ambacho kimegubikwa na hali mbaya ya kiutu huko Gaza.

https://p.dw.com/p/4dMr2
Ramadan  na Uislamu waumini wakiwa msikitini Indonesia
Waislamu wa Indonesia wafanya Tarawih, sala ya jioni kuashiria mkesha wa kwanza wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan. Picha: dapd

Saudi Arabia, ambayo ni sehemu ya maeneo matakatifu zaidi ya Uislamu, ilisema Jumapili kupitia shirika lake rasmi la habari la SPA kwamba Mahakama ya Juu ilitangaza "Jumatatu, Machi 11, 2024, ni mwanzo wa mwezi uliobarikiwa wa Ramadhani kwa mwaka huu".

Umoja wa Falme za Kiarabu na Qatar pia zilitangaza tarehe ya kuanza kwa Ramadhani kupitia vyombo vyao rasmi vya habari baada ya mwandamo wa mwezi.

Lakini awali kabisa, Iran ilitangaza kuwa mwanzo wa Ramadhani utakuwa Jumanne baada ya ofisi yake yenye dhima ya uchunguzi wa mwezi kusema haikuwezekana kuanza kwa kile ilichoelezwa kutoshuhudiwa kwa mwandamo wa mwezi.