Lavrov awasili Myanmar kwa mazungumzo na jeshi
3 Agosti 2022Matangazo
Tangazo la wizara ya mambo ya nje mjini Moscow limesema Lavrov atakutana na mwenzake wa Myanmar katika mji mkuu wa nchi hiyo uliojengwa na jeshi wa Naypyidaw, na kisha atafanya mazungumzo na viongozi wa nchi hiyo.
Lavrov yuko katika eneo hilo kuhudhuria mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Shirika la Mataifa ya Asia Kusini utakaofanyika nchini Cambodia, ambamo viongozi wa kijeshi wa Myanmar hawakualikwa.
Viongozi hao walilaaniwa na jumuiya ya kimataifa baada ya kuwauwa wafungwa wanne wa kisiasa, wakiwemo mbunge wa zamani na mwanaharakati wa demokrasia.
Urusi na China zimekuwa zikikosolewa kuwapatia silaha wanajeshi wanaoidhibiti Myanmar silaha za kuwakandamiza raia, tangu walipoiangusha serikali ya kiraia mwaka uliopita.