Kyiv yaidhinisha mswada wa kuwaajiri watu jeshini
11 Aprili 2024Huku wakikabiliwa na shinikizo kutoka kwa maafisa wa jeshi, wabunge waliondoa kipengele kwenye mswada huo ambacho kingewaruhusu askari walioko vitani kwa zaidi ya miezi 36 kurejea nyumbani.
Mswada huo unaohitaji kutiwa saini na Rais Volodymir Zelensky ili kuwa sheria, utaongeza adhabu kwa watakaokwepa kuajiriwa jeshini.
Zelensky: Ukraine imepata mafanikio katika utengenezaji wa makombora
Kyiv imekuwa na changamoto kwenye uwanja wa mapambano kwa miezi kadhaa, ikidhoofishwa na msaada unaohitajika kwa dharura wa Marekani ambao umezuiwa na Bunge, na uhaba wa askari na silaha.
Urusi ilifanya mashambulizi ya angani ya usiku kucha katika maeneo matano ya Ukraine, na kuwauwa watu wanne katika mji wa kusini wa Mykolaiv. Mashambulizi hayo yaliharibu kabisa kituo muhimu cha umeme karibu na Kyiv.
Akizungumza wakati wa ziara yake nchini Lithuania, Rais Zelensky amezihimiza nchi za Magharibi kutoyafumbia macho mashambulizi ya angani ya Urusi na kuipa Ukraine mifumo zaidi ya ulinzi wa angani.