Kura zaanza kuhesabiwa Rwanda baada ya uchaguzi mkuu
15 Julai 2024Hiyo ni baada ya kufanyika uchaguzi ambao rais wa sasa Paul Kagame akitarajiwa kwa kiasi kikubwa kupata ushindi na kuendelea kubakia madarakani kwa muhula mwingine wa miaka mitano.Wafahamu wagombea wawili wanaochuana na Kagame
Kagame anayeiongoza Rwanda tangu yalipomalizika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 na aliyechaguliwa kuwa rais mwaka 2000, anakabiliana na wapinzani wawili kwenye uchaguzi huo,Frank Habineza anayekiongoza chama cha Kijani na mgombea huru Phillipe Mpayimana.
Wakosoaji wake wengi wenye umaarufu walizuiwa kugombea kwenye uchaguzi huo.Zaidi ya wanyarwanda milioni tisa waliandikishwa kupiga kura katika vituo 2,433 vilivyowekwa nchi nzima. Shughuli ya kuhesabu kura ilipangwa kuanza mara moja baada ya vituo vya kupiga kura kufungwa alasiri kwa saa za Rwanda.Paul Kagame kusalia madarakani hadi mwaka 2034?