1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kura ya kumuondoa uongozini Trump kufanyika Jumatano

11 Januari 2021

Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria ya Bunge la Wawakilishi Marekani Jim McGovern amesema anatarajia kifungu cha kutaka kumuondoa madarakani Donald Trump, kiwasilishwe bungeni Jumatano ili kupigiwa kura na anatarajia kipite.

https://p.dw.com/p/3nn3J
USA Donald Trump und Mike Pence
Picha: Carlos Barria/REUTERS

Haya yanafanyika wakati ambapo mkewe rais Trump, Melania Trump amezungumza kwa mara ya kwanza kuhusiana na ghasia zilizotokea katika jengo la bunge la Marekani Jumatano iliyopita.

McGovern amesema ni muhimu wabunge wachukue hatua, ingawa ameweka wazi kwamba anatarajia wabunge wa Republican wakatae wito wa kuwasilishwa kwa kifungu cha kumtaka makamu wa rais Mike Pence atumie kifungu cha 25 cha katiba kumuondoa madarakani Trump. Pence na mawaziri watakuwa na saa ishirini na nne baada ya kura hiyo, kuamua iwapo waitumie ibara hiyo ya ishirini na tano.

McGovern amesema alichokifanya Trump ni kitu ambacho hakifiriki na anastahili kuwajibishwa.

Hatua nzuri anayostahili kuchukua Trump ni kujiuzulu

Haya yametokea baada ya spika wa bunge Nancy Pelosi kusema kuwa Trump ni sharti aondolewe madarakani kwa kuwa ni kitisho kwa demokrasia baada ya uvamizi uliofanyika katika majengo ya bunge maarufu kama Capitol Hill.

Streit um Mueller-Bericht : Kongresskammer erlaubt rechtliche Schritte gegen Trump-Regierung
Wabunge wa bunge la wawakilishi MarekaniPicha: picture-alliance/AP Photo/J. S. Applewhite

Seneta wa Pennsylvania Pat Toomey wa chama cha Republican ameungana na seneta mwenzake wa Alaska katika kumtaka rais huyo ajiuzulu.

"Nakiri kwamba huenda lisifanyike, ila nafikiri hiyo ndiyo hatua nzuri. Kwa sasa haionekani kana kwamba kuna nia au makubaliano ya kutumia ibara ya 25 ya katiba, na nafikiri hakuna muda wa kumuondoa uongozini, ukizingatia zimesalia siku kumi tu kabla rais aondoke, nafikiri jambo zuri kwa sasa ni kujiuzulu," alisema Toomey.

Wabunge Marekani wameonya kwamba Trump bado ana uwezo wa kufanya uharibifu mkubwa katika kipindi hiki cha siku kumi zilizosalia kabla kuapishwa kwa Joe Biden mnamo Novemba 20.

Melania anaiharibu Marekani kimya kimya

Wakati huo huo, mke wa rais Trump, Melania Trump amesema leo kuwa amevunjwa moyo na ghasia zilizofanywa katika jengo la Capitol Jumatano iliyopita na wafuasi wa mumewe. Akizungumza kwa mara ya kwanza, bi Trump amewashambulia pia wale ambao wametumia tukio hilo kusema mabaya kumuhusu.

USA I First Lady Melania Trump Visits New Hampshire
Mkewe Rais Trump, Melania TrumpPicha: Andrea Hanks/White House/ZUMA Wire/ZUMAPRESS/picture-alliance

Wiki iliyopita, rafiki yake wa zamani ambaye pia alikuwa msaidizi wake wa kwanza katika ikulu ya White House Stephanie Winston Wolkoff, aliandika aktika gazeti moja kwamba Melania, anahusika ila kimya kimya katika "kuharibiwa kwa Marekani."

Bi Trump pia amewataka Wamarekani kutotumia machafuko kuelezea hisia zao na pia kutowahukumu watu kutokana na rangi ya ngozi zao. Lakini hakuzungumzia jukumu la mumewe kuwachochea wafuasi wake kufanya maandamano kuelekea jengo la Capitol.