1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Kura ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa yaahirishwa

19 Desemba 2023

Kura ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya kusitisha mapigano katika ukanda wa Gaza imeahirishwa kutokana na mazungumzo yanayoendelea juu ya maneno sahihi yanayofaa kutumika kwenye rasimu ya azimio hilo.

https://p.dw.com/p/4aJzy
Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa juu ya azimio lisilo la kisheria la kusitishwa mapigano katika ukanda wa Gaza
Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa juu ya azimio lisilo la kisheria la kusitishwa mapigano katika ukanda wa Gaza mjini New York, MarekaniPicha: ANGELA WEISS/AFP

Mataifa ya Kiarabu yaliyowasilisha kura hiyo wanaitazama hatua hiyo kama ushahidi kwamba Marekani inazidi kukosa subra na mwenendo wa Israel katika ukanda wa Gaza.

Kura hiyo ilipaswa kufanyika jana saa kumi na moja alasiri mjini New York lakini imesogezwa mbele hadi leo.

Hata hivyo, badala ya kupinga tu azimio hilo moja kwa moja kama ilivyofanya awali, vyanzo vimeeleza kuwa Marekani huenda ikakubali "kusimamishwa" kwa mapigano.

Rasimu hiyo imewasilishwa na mataifa ya Kiarabu yakiongozwa na Umoja wa Falme za Kiarabu, na ambayo yametiwa moyo na uungwaji mkono mkubwa wa Umoja wa Mataifa wa kusitisha mapigano wiki iliyopita, wakati nchi wanachama 153 zilipopiga kura ya kuunga mkono azimio lisilo la kisheria la kusitisha mapigano huko Gaza.