Kundi La Taliban kushiriki mkutano wa Doha
16 Juni 2024Msemaji wa serikali hiyo Zabihullah Mujahid ameliambia shirika la habari la TOLO kwamba kundi hilo linaamini ushiriki wao katika mazungumzo ya Qatar utaifaidisha linapokuja suala la msaada wa kibinaadamu na masuala ya uwekezaji.
Mkutano huo utakaoandaliwa na Umoja wa Mataifa utafanyika tarehe 30 mwezi Juni hadi tarehe Mosi Julai ukiwa na nia ya kuongeza ushirikiano wa kimataifa na nchi hiyo inayokumbana na migogoro chungu nzima.
Afghanistan yawazuia wasichana kutoendelea na shule
Tangu kurejea madarakani kwa kundi hilo mwaka 2021, Taliban imekataa miito ya kuunda serikali inayojumuisha makundi yote ya kisiasa na kuhakikisha wanawake nchini humo wanapata haki ya elimu na pia kufanya kazi. Kufuatia hayo hakuna taifa hata moja lililoitambua serikali hiyo.
Fedha za nchi hiyo zimezuiliwa na mataifa ya Magharibi huku wakuu wa kundi la Taliban bado wakiwa katika orodha ya Marekani ya watu wanaotakiwa kukamatwa.