Kundi la G5 kuvunjwa rasmi
6 Desemba 2023Baada ya nchi nyingine tatu waasisi kujiondoa, nazo Chad na Mauritania zimesema katika taarifa kuwa zinafahamu na kuheshimu uamuzi wa uhuru wa Burkina Faso na Niger kuondoka katika muungano huo wa kijeshi, zikifuata nyayo za Mali.
Zimesema zitatekeleza hatua zote muhimu kwa mujibu wa mkataba ulioanzisha muungano wa G5.
Soma zaidi: Jeshi Burkina Faso lakemewa licha ya uungwaji mkono
Kundi hilo liliundwa mwaka wa 2014 lakini limepata matokeo machache tu.
Katika mwaka wa 2017, viongozi wa nchi hizo tano walikubaliana kuunda kikosi kazi cha pamoja cha kupambana na ugaidi kikiungwa mkono na Ufaransa.
Lakini watawala wa kijeshi wa Burkina Faso, Niger, na Mali wote wameituhumu Paria kwa kuwa na jukumu la kupitiliza baada ya miaka mingi ya kupelekwa vikosi vya Ufaransa kwenye nchi hizo.