Kuleba ziarani Beijing kutafuta amani nchini Ukraine
24 Julai 2024China inajipambanua kama mshirika asiyegemea upande wowote katika vita hivyo na kusema haitoi usaidizi hatari kwa pande zote mbili, tofauti na Marekani na mataifa mengine ya Magharibi. Hata hivyo, kuongezeka kwa ushirikiano wake "usio na ukomo" na Urusi kumesababisha wanachama wa NATO kuiita China kuwa "mwezeshaji madhubuti" wa vita vya Moscow, ambavyo serikali ya Beijing haijawahi kulaani.
Kuleba amesema atafanya mazungumzo ya kina na muhimu na waziri mwenzake wa China Wang Yi juu ya kufikia kile alichokiita "amani ya haki." Ziara ya Kuleba nchini China itakayokamilika Ijumaa, ni ya kwanza kufanywa na afisa yeyote wa ngazi ya juu wa Ukraine tangu Urusi ilipoivamia Ukraine Februari 2022.
Soma pia:Ukraine kuomba idhini pana ya kushambulia ndani ya Urusi
Beijing ilisema mazungumzo yatalenga mahusiano ya pande mbili na masuala mengine yenye maslahi ya pamoja.