Kosovo yaitaka Serbia kuwakabidhi washukiwa wa mashambulizi
25 Septemba 2023Waziri huyo ametoa wito, watu hao wakabidhiwe kwa mamlaka husika nchini humo.
Waziri huyo amewaambia waandishi wa habari kuwa Kulingana na taarifa walizo nazo hadi sasa, magaidi sita waliojeruhiwa wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Novi Pazar kusini mwa Serbia, na wanaiomba Belgrade kuwakabidhi mara moja kwa mamlaka ya Kosovo, ili waweze kukabiliwa na mkono wa sheria.
Marekani imelaani makabiliano hayo ya umwagaji damu kati ya wanajeshi wa Kosovo na watu wenye silaha karibu na mpaka wa Serbia. Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amezitolea wito Kosovo na Serbia kujiepusha na vitendo au kauli zinazoweza kuchochea zaidi hali hiyo.
Kosovo ilijitangazia uhuru wake kutoka kwa Serbia mwaka 2008 ingawa utawala wa Belgrade pamoja na washirika wake, China na Urusi bado hazitambui hatua hiyo ya Kosovo.