SiasaKosovo
Kosovo yafunga mpaka wake na Serbia kufuatia maandamano
28 Desemba 2022Matangazo
Serikali ya Kosovo ambayo zamani ilikuwa jimbo la Serbia ilijitangazia uhuru wake mwaka 2008, lakini Serbia imekuwa ikikataa kuutambua uhuru huo, na imekuwa ikiwahamasisha Waserbia wapatao 120,000 waishio ndani ya Kosovo kupinga mamlaka ya nchi hiyo mpya.
Maandamano ya hivi karibuni yalifanyika saa chache baada ya Serbia kutangaza kuwa majeshi ya nchi hiyo yamewekwa katika kiwango cha juu kabisa cha tahadhari wakati mivutano ikishamiri kati ya Belgrade na Pristina.
Sehemu nyingine mbili za mpaka baina ya mataifa hayo zimefungwa kufuatia maandamano yaliyoanza Desemba 10 mwaka huu.