Korti ya Venezuela yatoa waranti kukamatwa Edmundo Gonzalez
3 Septemba 2024Hatua hiyo imechukuliwa wiki moja baada ya wiki kadhaa za maandamano ya kuipinga serikali ya Rais Nicolas Maduro.
Mamlaka imesema imetoa hati hiyo baada ya Gonzalez kushindwa kufika mahakamani mara tatu kujibu maswali kutoka kwa waendesha mashtaka.
Kiongozi huyo wa upinzani Edmundo González, mwenye umri wa miaka 75, hajajitokeza hadharani tangu uchaguzi ulipomalizika.
Soma pia: Marekani yaikamata ndege ya rais wa Venezuela Nicolas Maduro
Mwendedesha mashtaka aliyetangaza hatua hiyo ya kukamatwa kwake amemlaumu kiongozi huyo wa upinzani kwa uhalifu ikiwa pamoja na mashtaka ya kula njama, kughushi hati na kutaka kupora mamlaka.
Mwanasheria mkuu wa Venezuela amesema mahakama imeikubali hati ya kukamatwa kwa kiongozi wa upinzani kutokana na madai ya kutenda uhalifu mkubwa.