Huenda likawa kombora la kushambulia bara moja hadi jengine.
18 Aprili 2019Jaribio hilo ambalo halikuonekana kama limekiuka masafa yaliyopigwa marufuku ya makombora ya nuklia imeliruhusu taifa hilo kuonyesha kwamba linaendelea na kutengeza silaha za nuklia na vile vile kuwahakikishia wakuu wa jeshi la nchini humo kuwepo kwa ishara za udhaifu wa kidipolomasia na Marekani.
Mchambuzi kutoka eneo la Korea Kazkazini alisema taarifa zilizoko katika vyombo vya habari katika taifa hilo zinatoa ishara ya kwamba silaha iliyojaribiwa ni kombora jipya ambalo linaweza kushambulia bara moja hadi jengine.
Taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa idara ya mambo ya Marekani katika wizara ya masuala ya kigeni ya Korea Kazkazini, ilimshutumu Pompeo kwa kudharua matamshi muhimu ya rais Kim Jong Un na vile vile kupuuza matakwa ya Korea Kazkazini ya kutaka mazungumzo ya Nuklia kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.
Taarifa hiyo ilimtaja Pompeo kama mtu wa kubuni mambo wakati katika hotuba yake siku ya Jumatatu alipopinga kauli ya Kim ya makataa ya mazungumzo ya Nuklia aliposema angependa mpango huo kukamilika hivi karibuni.
Korea Kazkazini inasema kuendelea kwa Pompeo kuwa katika mazungumzo hayo ni kuhakikisha kwamba mazungumzo hayo yanakorogeka hivyo basi kuitaka Marekani kumbadilisha na mtu mwengie aliye makini zaidi na mweledi wa mawasiliano.
Rais Kim kusafiri kwenda Urusi
Wakati huo huo Urusi ilisema rais wa Korea kazkazini Kim Jong Un atatembela taifa la Urusi mwishoni mwa mwezi huu wa nne. Taarifa fupi kutoka ikulu ya Urusi imethibitisha kwamba Rais Vladimir Putin amemualika Kim.
Ziara ya Kim Urusi itampa Putin nafasi ya kuwa mpatanishi katika mvutano huo wa muda mrefu wa silaha za Nuklia hivyo basi kuiinua hadhi ya Urusi katika masuala ya kikanda.
Vile vile Rais Putin atazuru China mwishoni mwa mwezi huu ambapo anatarajiwa kukutana na Kim katika mji wa bandari wa Vladivostok karibu na mpaka wa Korea Kazkazini.
Baadhi ya wachambuzi wanasema kitendo cha Korea Kazkazini kufanya majaribio ya makombora ya nuklia ni njia ya kuilazimisha Marekani kuacha msimamo wake mgumu na kukubaliana na matakwa ya Koerea kazkazini ya kuwaondolea vikwazo vya kimataifa.
Wiki jana Kim alisema yuko tarayi kwa mkutano wa tatu na rais Donald Trump ila akaweka makataa ya mwisho wa mwaka huu kwa Marekani kutoa matakwa ya kukubalika juu ya mpango huo.
(APE)