Ushirikiano kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini matatani
16 Januari 2024Matangazo
Kitisho hicho kinatokea wakati Pyongyang ikiyavunja mashirika yanayoshughulikia ushirikiano na mazungumzo kati yake na Korea Kusini.
Shirika la habari la Korea Kaskazini KCNA limeripoti kuwa, Kim Jong Un amesema hatotambua mpaka wa bahari kati ya nchi hizo mbili na amependekeza kufanyike mabadiliko ya katiba ili kuiruhusu nchi hiyo "kuikalia" Seoul.
Ama kwa upande wa Korea Kusini, Rais Yoon Suk Yeol ameliambia baraza lake la mawaziri kuwa, iwapo Korea Kaskazini itaendelea na uchokozi wake, basi nchi yake itajibu vikali na kuashiria uwezo mkubwa wa jeshi lake wa kukabiliana na vitisho vya aina yoyote.