1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Korea Kaskazini yatishia satelaiti za kijasusi za Marekani

2 Desemba 2023

Korea Kaskazini imeionya Marekani kwamba itaharibu satelaiti za kijasusi za taifa hilo ikiwa serikali yake itajaribu shambulio lolote kwa vifaa vyake kwenye eneo lake la anga.

https://p.dw.com/p/4Zhff
Nordkorea Sonderwirtschaftszone Rason
Picha: YONHAPNEWS AGENCY/picture alliance

Korea Kaskazini imeionya Marekani kwamba itaharibu satelaiti za kijasusi za taifa hilo ikiwa serikali yake itajaribu shambulio lolote kwa vifaa vyake kwenye eneo lake la anga.

Onyo hilo linatolewa baada ya Pyongyang kurusha angani satelaiti yake ya kwanza ya uchuguzi wake wa kijeshi juma lililopita.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika la habari la umma la Korea ni kwamba wizara ya ulinzi ya Korea Kaskazini itachukulia hatua hiyo kama tangazo la vita.

Kauli hiyo inafuatia matamshi ya afisa wa Marekani kwamba Washington haikubaliani na kile walichokiita uwepo wa adau katika eneo la anga na inaweza kutumia mbinu mbalimbali kuzuia, ikimaanisha mafanikio ya kurushwa kwa satelaiti ya kijasusi ya Korea Kaskazini kuliko fanyika mwishoni Novemba.