SiasaAsia
Korea Kaskazini yathibitisha kurusha kombora
7 Januari 2025Matangazo
Mamlaka inayohusika na makombora imesema kwenye taarifa iliyotolewa jana kwamba imefanikiwa kufanya majaribio ya aina mpya ya kombora hilo ambalo kasi yake inazidi kasi ya sauti.
Shirika la habari la Korea Kaskazini, KCNA, imesema kwenye taarifa yake ya leo kwamba kombora hilo lilifika umbali wa kilomita 1,500, na kwamba jaribio hayo yalisimamiwa na kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong Un.
Soma zaidi: Zelenskiy adai wanajeshi wa Korea Kaskazini wanauawa kwa wingi
Kim amenukuliwa na KCNA akisema wameamua kuunda kombora lenye uwezo huo kukabiliana na vitisho vya wale aliowaita "vikosi vya maadui wa dola."
Kurushwa kwa kombora hilo kunasadifiana na ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, kwenye eneo hilo.