1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Korea kaskazini yasema ndege ya Marekani imeingia anga yake

18 Agosti 2023

Jeshi la Korea Kaskazini limesema limeziweka tayari ndege zake za kijeshi baada ya ndege moja ya upelelezi ya Marekani kuingia katika anga yake.

https://p.dw.com/p/4VKbQ
Korea Kaskazini imetaja hatua hiyo kuwa "uchokozi hatari wa kijeshi". (Picha ya maktaba)
Korea Kaskazini imetaja hatua hiyo kuwa "uchokozi hatari wa kijeshi". (Picha ya maktaba)Picha: picture-alliance/dpa

Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari la Korea Kaskazini la KCNA siku ya Ijumaa.

Msemaji wa jeshi la Korea Kaskazini ambaye hakutajwa jina amesema tukio hilo ni "uchokozi hatari wa kijeshi" na jamhuri hiyo inatafakari kuchukua hatua ili kuzuia kurudiwa kwa tukio hilo katika siku zijazo.

Tukio hilo limefanyika wakati ambapo Rais Joe Biden wa Marekani anajiandaa kukutana na viongozi wa Japan na Korea Kusini huko Camp David, Maryland.