JangaKorea Kaskazini
Korea Kaskazini yakumbwa na maafa makubwa ya mafuriko
31 Julai 2024Matangazo
Hayo yametangazwa na shirika la habari la nchi hiyo usiku wa kuamkia leo KNCA. Shirika hiyo limeripoti kwamba mji wa Sinuiju na kaunti ya Uiju iliyo karibu na mpaka na China ndio maeneo yaliyoathiriwa zaidi na janga hilo.
Ekari 7,400 pamoja na majengo ya umma na barabara vimefunikwa kwa maji. Maafa hayo yalipelekea kuitishwa kikao cha ngazi ya juu chama tawala cha kikomunisti mapema wiki hii chini ya kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un.
Kim alielezea kufadhaishwa na uharibifu uliotokea na kutoa mwito wa kufanyika jitihada za haraka kurejesha hali ya kawaida kwenye maeneo yaliyoathika. Kiongozi huyo alikwishalitembelea mwenyewe eneo la maafa mnamo Jumapili iliyopo.