Korea kaskazini yaikosoa Marekani kwa msaada wake, Ukraine
29 Aprili 2024Hapo jana Jumapili, mkurugenzi wa idara ya mambo ya nje kuhusu masuala ya kijeshi katika wizara ya ulinzi wa kitaifa ya Korea Kaskazini, alinukuliwa katika taarifa akisema kuwa Marekani imesambaza kisiri makombora hayo kwa Ukraine na kuzua wasiwasi katika jamii ya kimataifa.
Korea Kaskazini yasema Marekani haiwezi kulishinda jeshi la Urusi
Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa Marekani haiwezi kulishinda jeshi la Urusi na watu wake kwa aina yoyote ya silaha za kisasa ama msaada wa kijeshi.
Soma pia: Marekani yapitisha msaada wa dola bilioni 61 kwa Ukraine
Mnamo Aprili 24, afisa mmoja wa Marekani alisema kuwa katika wiki za hivi karibuni zaidi, nchi hiyo ilisafirisha kisiri makombora ya masafa marefu kuelekea Ukraine kwa matumizi katika vita vyake na Urusi.
Ushirikiano wa kijeshi kati ya Korea Kaskazini naUrusiunaimarika, hali inayoonekana na Marekani na washirika wake kama ongezeko la mvutano katika rasi ya Korea.