Korea Kaskazini yafanya jaribio la kombora la masafa marefu
12 Julai 2023Jaribio hilo la kombora lililofyetuliwa kwenye pwani ya mashariki mwa nchi hiyo, limefanyika baada ya Korea Kaskazini kuituhumu Marekani kukiuka sheria za kimataifa kwa kutuma ndege zake za ushushushu juu ya anga yake pamoja na safari ya hivi karibuni ya nyambizi ya jeshi la Marekani yenye makombora ya nyuklia nchini Korea Kusini.
Inaarifiwa koMarekani na Korea Kusini zafanya luteka ya pamojambora lililojaribiwa leo ndiyo la masafa marefu zaidi kuwahi kufyetuliwa na Pyongyang ambapo lilisafiri umbali wa kilometa 1,000 kwa dakika 74 huku likiwa kilometa 6,000 angani.
Rais Yoon Suk Yeol wa Korea Kusini aliye nchini Lithuania kuhudhuria mkutano wa kilele wa NATO aliitisha kikao cha dharura kujadili jaribio hilo na baadaye atakutana na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida kujadili wasiwasi wa usalama kwenye eneo lao.