Kongo yaishutumu Apple kwa matumizi ya ''madini ya damu''
25 Aprili 2024Shirika la habari la AFP limeripoti kuwa mawakili hao wenye makaazi yao mjini Paris nchini Ufaransa, wameitumia kampuni hiyo ilani rasmi ya kuitaka isitishe mara moja shughuli hiyo na kuionya kuwa huenda ikachukuliwa hatua za kisheria iwapo itaendelea kufanya hivyo.
Mawakili hao wameishtumu Apple kwa madai ya kununua madini yaliongizwa nchini Rwanda kutoka Kongo kinyume cha sheria ambapo baadaye husafishwa na kuingizwa katika soko la kimataifa.
Ikionesha taarifa ya ripoti yake ya mwaka 2023 kuhusu madai ya matumizi ya kile kinachotajwa kuwa madini ya migogoro ambayo ni muhimu kwa kutengeneza bidhaa za gharama ya juu, Apple, imeiambia AFP kwamba haijapata sababu zozote za kimsingi kuhitimisha kuwa madini yoyote yanayodaiwa kutumika kwa bidhaa zake kufikia tarehe 31 mwezi Desemba mwaka 2023 yalitumika kwa njia yoyote ile kufadhili ama kunufaisha makundi yenye silaha nchini Kongo ama katika nchi jirani.