Kongo yaanzisha mazungumzo na Zambia kufungua mpaka
12 Agosti 2024Mnamo siku ya Jumamosi, Waziri wa Biashara wa Zambia Chipoka Mulenga alitangaza kuufunga kwa muda mpaka huo baada ya kuzuka maandamano kwenye mji wa mpakani wa Kasumbalesa. Maandamano hayo yalifanywa na wasafirishaji bidhaa waliokuwa wakipinga uamuzi wa Kongo wa kuzuia kuingizwa vinywaji na vileo kutoka Zambia .
Taarifa iliyotolewa na wizara ya biashara ya Kongo, imesema mazungumzo kati ya serikali ya nchi hiyo na Zambia yanafanyika ili kuwezesha kufunguliwa kwa eneo hilo la mpaka haraka iwezekanavyo.
Soma pia: Zambia yaagizia maelfu ya tani za mahindi kutoka Tanzania
Wawakilishi wanapanga kukutana mjini Lubumbashi kutafuta suluhisho la kudumu juu ya mahusiano ya kibiashara kati nchi ya nchi hizo jirani.
Kongo iliyo mzalishaji mkubwa wa pili duniani wa madini ya shaba inatumia njia za mataifa jirani ikiwemo Zambia kusafirisha malighafi hiyo kimataifa.