1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiAfrika

Kongo: Walimu wagoma wakitaka mazingira bora ya kazi

Admin.WagnerD2 Septemba 2024

Waalimu wa shule za msingi katika majimbo ya Kivu Kusini na Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamesusia kufundisha leo wakidai kuboreshewa mshahara poamoja na mazingira bora ya kazi.

https://p.dw.com/p/4kAyI
Elimu | Wanafunzi wakiwa darasani
Wanafunzi wa darasa la awali wakiwa darasaniPicha: Issouf Sanogo/AFP/Getty Images

Hatua ya walimu kuanzisha mgomo ni kufuatia mkutano kati ya wajumbe wa serikali kuu mjini Kinshasa na wawakilishi wa vyama mbalimbali vya walimu wa shule za kiserikali na shule za madhehebu mbalimbali yaliyoidhinishwa na Serikali ya Kongo yaani SYECO, SYNECATH, SYNEP na kadhalika uliofanyika mnamo Agosti huko Bibwa mjini Kinshasa ambako walimu walidai mshahara unowaruhusu kujikimu kimaisha, wakibainisha kwamba tangu Serikali itangaze mpango wa elimu bilöa malipo kwa shuile za msingi, shughuli nyingi za kboresha elimu katika taasisi hizo zimezorota.

Jacques Cirimwami ni Msemaji wa Muungano wa vyama vya Walimu wa Kivu Kusini, akiwa pia mratibu wa vyama vyote vya walimu katika mikoa yote ya Kongo ameiambia Dw kwamba bado serikali haijatoa majibu yenye tija katika kufikia suluhu ya changamoto inayoshuhudiwa sasa.

Soma pia:Uingereza yakabilliwa na mgomo mkubwa wa sekta ya umma

Mapema asubuhi ya leo katika majimbo mbalimbali nchini Kongo yakiwemo Kivu Kusini, wanafunzi waliovaa sare mpya za masomo waliwasili mashuleni, ikiwa ni siku ya kwanza baada ya likizo ya mwaka, lakini walimu walisusia kufundisha na wengine hawakufika kabisa katika vituo vyao vya kazi.

Hali hii pia ilishuhudiwa katika majimbo ya Kivu Kaskazini, katika mji wa Goma ambapo vijana wenye hasira walizuia madereva wa magari kuwapeleka watoto shuleni, huko Equateur, huko Ituri, Tanganyika, na majimbo mengine ya Kongo.

Wazazi Walimu rejeeni shuleni

Baadhi ya wazazi ambao watoto wao wameripoti shuleni kwa mara ya kwanza wamewasihi walimu kutumia njia mbadala katika kushinikiza matakwa yao kwa serikali na si kususia masomo.

Kituo cha elimu ya awali kwa watoto wakimbizi

Wamesema hatua hiyo inaleta usumbufu wa kisaikolojia kwa wanafunzi wapya ambao walitarajia kukutana na waalimu wao kwa mara ya kwanza lakini mambo yamekwenda tofauti na matarajio yao hatua ambayo inaweza kuwatatiza wanafunzi kisaikolojia.

Naomi Muteza ni mzazi aliyewasindikiza watoto wake shuleni mjini Bukavu, anaelezea mafadhaiko akisema walimu wanafanya mgomo wakati wazazi wengi wametatizika katika mazingira magumu kiuchumi ili kupata baadhi ya vifaa vya shule.

Soma pia:Walimu na Madaktari wa Zimbabwe wagoma

Kwa upande wake Olivier Mushagalusa ni mwanachama wa Chama tawala cha UDPS mjini Bukavu, anaonya walimu kuzingatia nia nzuri ya Serikali ya Kongo wakati huu katika kuboresha elimu na kusaidia wanafunzi ambao wazazi wao wana uwezo mdogo kiuchumi katika kumudu shule za kulipia.

Licha ya mgomo wa walimu, serikali ya Kongo inasema mwaka mpya wa shule tayari umeanza.

Waziri wa Nchi anayeshughulikia Elimu ya Taifa na Uraia Mpya, Raïssa Malu awataka walimu, wazazi na wanafunzi kuchukua tahadhari zote ili kupambana na ugonjwa wa mpox.