1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kongamano la G7 Elmau, Ujerumani: Je ni zaidi ya onyesho?

27 Juni 2022

Viongozi wakundi la G7 wanataka kukabiliana na mzozo wa hali ya hewa, njaa na vita. Lakini je hilo liko ndani ya uwezo wao? Wapinzani 900 wa kundi hilo wamekusanyika nchini Ujerumani kwa maandamano dhidi ya G7

https://p.dw.com/p/4DIa3
Deutschland G7 Gipfel Protest
Picha: Lukas Barth/REUTERS

Muungano wa ' Simamisha G7 Elmau' uko hapa kupinga mamlaka ya wakuu saba wa nchi na serikali, ambao maamuzi yao yana ushawishi mkubwa. Ni asilimia 10 tu ya idadi ya watu duniani wanaishi katika mataifa hayo saba yaliostawi kiviwanda yaliounda kundi la  G7 kwa njia isiyo rasmi katikati ya miaka ya 1970. Lakini maamuzi yao, ingawa hayafungi kisheria, yanaathiri asilimia 90 ya watu wengine kote duniani.

Wanaharakati wanadaia mataifa mengine yanatumiwa kama mpango mbadala

Mwanaharakati Christopher Olk anasema eneo la Kusini la dunia halina sauti hapo. India, Argentina, Senegal na Afrika Kusini ambazo zimealikwa katika siku ya pili ya kongamano hilo zimealikwa tu kwasababu zina raslimali asili inayohitajika wakati ambapo kuna upungufu wa nishati katika eneo tajiri la kaskazini. Mwanaharakati mwingine kutoka Uganda anazungumza kwa uchungu akisema, bara la Afrika halipaswi kutumiwa kama mpango mbadala wa kundi hilo la G7 linalohitaji nishati kwa kiasi kikubwa. Wazungumzaji wengine wanaonya juu ya kuongezeka kwa vita vya Ukraine na mzozo wa hali ya hewa. Mwanaharakati mwengine anasema kuwa hawatawaruhusu kuharibiwa sayari ya dunia na maisha ya siku za baadaye.

Deutschland G7 Gipfel Protest
Wanaharakati waandamana nje ya wizara ya fedha ya Ujerumani kutaka msamaha wa deni kwa nchi za kusini mwa duniaPicha: Christian Mang/REUTERS

Mchana wa siku ya kwanza ya mkutano huo, mashirika manne yanayohusika hasa na kupunguza umaskini, afya na ulinzi wa hali ya hewa, yalialika umma kwenye mkutano na waandishi wa habari katika kituo cha vyombo vya habari. Mashirika hayo manne Global Citizen, Oxfam, World Vision na ONE ni miongoni mwa wakosoaji wa G7, lakini tofauti na waandamanaji wengine hawahoji iwapo unapaswa kuwepo kabisa au la. Scherwin Saedi wa shirika la ONE Germany, anasema ni vyema na muhimu kwa wakuu wa nchi na serikali kuzungumza na kujadiliana wao kwa wao, lakini pia lazima watimize ahadi

Lakini suluhisho linaweza kupatikana vipi bila ya kugonganisha mgogoro mmoja na mwingine?

Shirika la Global Citizen linamshutumu kansela wa Ujerumani Olaf Scholz kwa kujaribu kufifisha mikataba ya ulinzi wa hali ya hewa ya kimataifa. Shirika la ONE linasema katika kongamano hilo, hakuna yeyote atakayedanganywa kwa maneno ya ukarimu likiongeza kuwa wakati wa kongamano lililopita la G7 nchini Ujerumani, ahadi nyingi zilitolewa lakini hakuna matokeo makubwa na kwamba hawawezi kuruhu G7 kuepuka hilo.