1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoMalawi

Kocha wa timu ya taifa Malawi afutwa kazi

3 Aprili 2023

Timu ya taifa ya Malawi imemfuta kazi kocha wake raia wa Romania Mario Marinica baada ya kufungwa mabao 4-0 na Misri katika mechi ya kufuzu mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON.

https://p.dw.com/p/4PeLQ
Africa Cup of Nations Malawi vs Senegal
Mchezaji wa timu ya taifa ya Malawi Gabadihno Mhango (kuhsoto) wakati wa mchezo na Senegal uliopigwa mwaka jana.Picha: Pius Utomi Ekpei/Getty Images/AFP

Kipigo hicho cha aibu mjini Lilongwe, mji mkuu wa nchi hiyo ya Kusini mashariki mwa Afrika, imeiacha timu hiyo ya taifa ikiwa na matumaini madogo ya kufuzu mashindano hayo yatakayofanyika nchini Ivory Coast.

Marinica mwenye umri wa miaka 58, alikuwa akishirikiana na Meck Mwase na sasa kumetolewa miito kwa naibu wake huyo ambaye ni raia wa Malawi kuchukua nafasi ya Kocha Mkuu wa timu hiyo inayoshikilia nafasi ya 124 katika viwango vya ubora wa soka duniani FIFA.

Malawi, iko katika nafasi ya tatu kwenye Kundi D linalojumuisha pia vinara Misri, Guinea na Ethiopia inayoshikilia nafasi ya mwisho. Hata hivyo, ili kufuzu mashindano ya AFCON, itawalazimu kupata ushindi ugenini dhidi ya Ethiopia katika mechi itakayochezwa mwezi Juni na Guinea mwezi Septemba.