Kiwewe cha dhahabu Kewanja, Tanzania
21 Februari 2013Lakini hadi sasa utajiri wa madini hayo haukuwanufaisha wananchi kutokana na kwamba migodi hiyo iko kwenye mikono ya makampuni ya kimataifa. Mwishoni mwa miaka ya 1990 serikali ya nchi hiyo imezivutia kampuni hizo za migodi kwa kupunguza kodi na leseni zake kuwa rahisi.
Hata hivyo kunakuwepo na mizozo kwenye sehemu nyingi za migodi kati ya kampuni hizo na wananchi wenyeji. Hususan hali hiyo imejitokeza kwenye mkoa wa Mara Kaskazini ulioko magharibi kabisa ya eneo la kaskazini magharibi mwa Tanzania kwenye mpaka na Kenya.Hapo kila kitu kinahusiana na dhahabu na kwamba kwa gramu chache tu za dhahabu watu wanakuwa tayari kuhatarisha maisha yao.
Wafanyakazi wavamizi
Wanasema wakati ni dhahabu ni masafa ya kama nusu saa kwa mwendo wa gari kutoka kijiji cha Kewanja hadi mpaka wa Kenya. Jumanne anauparamia mlima mkubwa wa kifusi cha migodi akiwa kama mita chache tu kufika juu. Kijana huyu ni mvamizi kwa sababu mlima wa vifusi aliokuwa ameuparamia unamilikiwa na kampuni ya dhahabu ya African Barrick Gold (ABG) tawi la kampuni kubwa kabisa ya kuzalisha dhahabu duniani ya Barrick Gold kutoka Canada. Mawe yalioko katika mlima huo ni taka kutoka kwenye mgodi ulio karibu ambapo hata hivyo huwa chini ya ulinzi wa kampuni hiyo.
Kwa wananchi wengi wanaoishi katika kijiji cha Kewanja katika mkoa wa Mara Kaskazini masalia hayo ni pato pekee kwao. Kila siku huuvamia mlima huo wa kifusi mara kwa mara kwa matarajio ya kupata mabaki kidogo ya dhahabu.
Kwa mujibu wa Jumanne mtu mmoja kati ya kila watu watatu ni mvamizi mahala hapo. Wengi kati yao ni vijana wa kiume na kuna na hata watoto. Jumanne ana umri wa takriban miaka 20 na huuza dhahabu anayoipata katika soko la kijiji ambapo hujipatia laki mbili za Tanzania kwa mwezi sawa na euro mia moja, kwa hiyo Jumanne ni miongoni mwa watu wanaojipatia kipato kikubwa katika mkoa huo.
Kuhatarisha maisha
Hata hivyo Jumanne anasema mzungu akimaanisha wamiliki wa mgodi huo amekuwa akiwabana sana wasichukue mawe yalioko kwenye mlima wa kifusi cha mgodi na kwamba watu wengine hupoteza maisha yao lakini maisha ni magumu na hawana njia nyengine ya kujipatia kipato.
Eneo la kampuni hiyo ya dhahabu huwa liko chini ya ulinzi mkali ambapo hata polisi wa taifa hushiriki katika kutowa ulinzi huo. Walinzi hao huwa na mabomu ya kutowa machozi, risasi za mpira na na silaha nyengine kali. Kila mara watu huuwawa na wengine kujeruhiwa. Mwaka 2012 pekee kutokana na vyombo vya habari vya ndani ya nchi takriban watu wanane wameuwawa karibu na mgodi huo au kwenye mgodi wenyewe. Kwa wavamizi hasira inazidi kupanda ambapo mvamizi mmoja aliekataa kutaja jina lake amesema hakuna mtu anayejali juu ya watu walioko hapo na dio maana hupigwa risasi kama mbwa kwamba polisi hutekeleza kila wanachoagizwa na kampuni na wanakuwa kama vile ni vibaraka wao.
Donge nono
Kwa upande mwengine fedha nyingi hupatikana kutoka kwenye milima hiyo ya vifusi vya migodi. Mgodi huo wa Mara Kaskazini umekuwa na wamiliki mbali mbali hapo mwaka 2006 ulikuwa nchini ya mikono ya AGB. Kampuni hiyo zaidi ya muongo mmoja uliopita imekuwa ikijishughulisha nchini Tanzania na kwa hivi sasa pia inashughulikia migodi mengine minne ya dhahabu nchini humo.
Huko Mara Kaskazini kwa mujibu wa taarifa za kampuni hiyo wafanyakazi wa migodi 360 moja kwa moja wanatoka katika maeneo hayo na wengine zaidi ya 1,500 wakaazi wa hapo wanafanya kazi kwa njia ya mikataba na kampuni hiyo. Haata hivyo hiyo haiwezi kuitwa miujiza ya kazi. Mgodi huo hutowa ajira chache tu kwa wanakijiji 70,000 waliokuwepo kwenye vijiji vilio karibu na mgodi huo. Ingawa kampuni za migodi hupata fedha nyingi lakini hutowa ajira chache hili ni tatizo halisi katika sekta ya malighafi. Kwa mwaka 2001 pekee kampuni hiyo ya ABG imejipatia zaidi ya euro milioni 200 kutoka mgodi wake huo wa Mara Kaskazini.
Miradi ya kijamii
Gary Chapman meneja wa mgodi anasema bila ya shaka kampuni hiyo inatakiwa kuwajibika kwa jamii na kwamba wanachukua hatua kujenga uaminifu baina yao na jamii ili kuheshimiwa na kuthaminiwa na jamii kwa nia ya kushirikiana na kuleta maendeleo. Kutimiza lengo hilo kampuni hiyo ina kitengo cha kushughulikia uhusiano na umma huko Mara Kaskazini ambacho kinaundwa na wafanyakazi 17 wa kiume na wa kike. Wafanyakazi hao wa masuala ya jamii hufanya ziara vijijini na kuwasiliana na wakuu wa vijiji na watu wenye kushughulikia jamii. Kitengo hicho kinasimamia miradi ya jamii ya kampuni hiyo. Kitu kimoja ambacho kampuni ya African Barrick Gold inajivunia sana ni shule ya sekondari ya Ingwe ambayo iko dakika chache kwa mwendo wa gari kutoka mgodi wao.
Kwa madarasa ambayo yamechakaa kampuni hiyo ya ABG imeyafanyia ukarabati hapo mwaka 2012 na hivi sasa wanashughulikia ujenzi wa ukumbi wa chakula na majengo zaidi ya shule kwa kutumia kampuni za kijenyeji kwa lengo la kuzalisha ajira zaidi. Hili ni jambo linalolitiliwa mkazo na kampuni hiyo ya AGB. Joash Mageka mkuu wa shule hiyo anafurahia mabadiliko mazuri kwana shule hiyo sasa inapendeza na kwamba pia idadi ya wanafunzi wanaokwenda kufanya kazi kama wavamizi imepunguwa. Anasema ingawa bado kuna wengine wanaoendelea kwenda wanajaribu kuwaelimisha juu ya umuhimu wa elimu na vipi inaweza kuwasaidia katika maisha yao ya baadae. Shule hiyo ni mradi wa kupigiwa mfano na kwa kampuni hiyo huo ni mfano wa maendeleo ya mkoa huo.
Mkoa unaendelea
Kwa mujibu wa taarifa za kampuni hiyo mwaka 2010 kampuni ya AGB imetowa dola milioni 20. 6 kwa ajili ya miradi ya jamii nchini kote Tanzania. Kiwango hiki ni chini ya aslimia moja ya faida inayopata kampuni hiyo. Idara ya uhusiano na umma ya kampuni hiyo inasema sehemu kubwa ya fedha hizo zimepelekwa Mara Kaskazini. Lakini hilo limetokea miaka miwili tu iliopita.Kwa nini halikufayika mapema zaidi hakuna mtu anayetaka kufafanuwa hilo.
Kwa mujibu wa Zakayo Kalebo meneja wa uhusiano wa jamii wa kampuni hiyo idadi ya nyumba imeongezeka na pikipiki zimejaa na kimsingi watu wanauona mgodi huo kuwa na manufaa kwa sababu maendeleo makubwa yameweza kufikia hali ambayo haikuwa hivyo kabla ya kuwepo kwa mgodi huo.
Kusema kwamba hali hiyo imesaidia kukuza uchumi au kusema ni neema ya mali ghafi itakuwa kama ni kutia chumvi kwa Mara Kaskazini. Biashara ya dhahabu huwavutia watu wengi kutoka nje. Kwa mfano David Arumba aliigia hapo mwaka uliopita kutoka nchi iirani ya Kenya ana umri wa miaka 25 ni mtu pekee katika familia yake aliekwenda shule. Lakini haafiki kufanya kazi za uvamizi na ameamuwa kuwa na kazi tafauti. Anasema watu wengi wanaokwenda hapo huishia kupigwa risasi na wengine kujeruhuiwa.
Yeye hakutaka kuwa kwenye matatizo ya kufukuzana na polisi na kuwepo mahala ambapo hakustahiki.Ameamua kuwa na biashara ya kuosha magari kwa kuwa inampa uhuru.
Kijana huyo ana sehemu ndogo ya kuosha magari katika kijiji cha Kewanja na mke wake humsaidia kwa kuuza ndizi na mafuta ya petroli katika chupa za plastiki.Wengi ya wanavijiji hao wanaishi kwa kutegemea pungufu ya dola moja kwa siku na kuweza kuwa na maji na umeme ni vitu vya anasa.
Nini tatizo Mara Kaskazini ?
Sospeter Muhongo ni waziri wa madini wa Tanzania mwenyewe anatoka Mara Kaskazini ni mwanaeleojia na amekuwa katika wadhifa huo kwa miezi kadhaa. Ameongeza kodi kwa kampuni hizo na amekuwa akitaka zijihusishe zaidi na miradi ya kusaidia jamii.Muhongo anasema wamejaribu na hawatosita watafanya juhudi zote kuhakikisha kwamba kuna amani na usalama katika eneo hilo. Anaona njia moja ya kulitatua tatizo hilo ni kuwekeza katika elimu ambapo watu watakapokuwa wamejifunza na kuelimika vizuri watakuja kuwa na fikra tafauti.
Lakini hadi sasa hakuna ishara ya kuwa na fikra tafauti katika kijiji cha Kewanja mkoa wa Mara Kaskazini. Biashara hiyo haramu ya dhahabu hufanyika kwa vificho na mawe kuvunjwa vipande vipande kuichuja dhahabu huko vijijini. Juu ya kwamba utaratibu wa kuisafisha dhahabu hiyo huhusisha matumizi ya zebaki ambayo ni hatari kwa afya lakini hivyo ndivyo anavyofanya Jumanne ambaye anasema binaadamu lazima atambuwe wapi anaweza kupata riziki yake kwani fedha anazoweza kupata kwa siku moja inabidi asubiri kwa mwaka mzima kuweza kuzipata akijishughulisha na kilimo.
Kidonge cha dhahabu kinachong'ara kwenye mkono wake pengine hakizidi hata gramu moja. Huuzwa kwa Euro 20 kwenye soko la magendo. Ni sehemu ndogo ya utajiri wa mali ghafi lakini ni fedha nyingi kwa maskini walioko kaskaziini mwa Tanzania.
Mwandishi: Julia Hahn/Mohamed Dahman
Mhariri:Yusuf Saumu