Kiwanda pekee cha kuzalisha umeme Gaza chafungwa
11 Oktoba 2023Hii ni kufuatia Israel kusitisha usambazaji wa nishati kufuatia mashambulizi makubwa yaliyofanywa na kundi la wanamgambo la Hamas.
Kampuni ya Umeme ya Palestina ilikuwa imetahadharisha awali kwamba iko katika hatari ya kusitisha uzalishaji.
Kampuni hiyo lakini imesema Ukanda wa Gazabado utakuwa unapata umeme kutokana na nishati ya jua ingawa usambazaji utakuwa kwa masaa kumi tu kila siku.
Hayo yakiarifiwa Israel imeendelea kuishambulia Gaza na kusababisha uharibifu mkubwa wa majengo wakati ambapo wanajeshi wake wamewapata wahanga zaidi wa mashambulizi ya Hamas, siku tano baada ya kundi hilo kuishambulia Israel.
Soma pia:Papa Francis airai Hamas kuwaachia mateka, aeleza wasiwas mzingiro Gaza
Jeshi la Israel limesema limegundua miili 1,200, sehemu kubwa ya miili hiyo ikiwa ya raia waliokuwa hawakujihami huku maafisa wa Gaza wakiripoti zaidi ya miili elfu moja ya watu waliouwawa.
Rais wa Marekani Joe Biden ameahidi kupeleka silaha na vifaa vya kijeshi kwa mshirika wake Israel.
Marekani, Umoja wa Ulaya, Ujerumani ikiwemo, pamoja na nchi nyengine zimeliorodhesha kundi la wanamgambo la Hamas katika orodha ya makundi ya kigaidi.