1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kipchoge: "sio kila siku ni Krismasi"

3 Machi 2024

Bingwa mara mbili wa Olimpiki wa Kenya Eliud Kipchoge anena baada ya maandalizi yake ya Michezo ya Paris kugonga mwamba.

https://p.dw.com/p/4d7NZ
Mwanariadha wa Kenya Eliud Kipchoge
Mwanariadha wa Kenya Eliud KipchogePicha: Christoph Soeder/AP

Kipchoge mwenye umri wa miaka 39 alififia vibaya katika umbali wa kilomita 20 na kumaliza mbio hiyo kwa muda wa saa 2 dakika 6 sekunde 50. Baada ya mbio, alisema kwamba kuna "kitu kilifanyika katikati ya mbio", bila kufafanua zaidi.

Benson Kipruto wa Kenya alishinda kwa rekodi ya kutimkwa kwa saa 2:02:16 mbele ya Timothy Kiplagat  na Vincent Ngetich wote kutoka Kenya.

Mbio hizo zinafanyika chini ya mwezi mmoja baada ya mshikilizi wa rekodi ya dunia Kelvin Kiptum kufariki wakati gari lake lilipogonga mti nchini Kenya.

Hata hivyo Kipchoge atajaribu kushinda medali yake ya tatu ya dhahabu katika mbio za marathon za Olimpiki baadaye mwaka huu na alisema "ni mapema mno kusema" atakuwa katika hali gani wakati wa Mashindano ya Paris.