1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Abbas akutana na Gantz Ramallah

30 Agosti 2021

Kiongozi wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas amekutana na mwakilishi wa ngazi ya juu wa serikali ya Israel, mkutano huo ukiwa wa kwanza kufanyika kwa muda mrefu baina ya wawakilishi wa nchi hizo mbili.

https://p.dw.com/p/3zfbN
AFP Bildkombo Mahmud Abbas  Benny Gantz
Picha: Thaer Ghanim/Menahem Kahana/AFP

Ofisi ya Waziri wa Ulinzi wa Israel Benny Gantz imethibitisha katika taarifa kuwa, waziri huyo wa ulinzi alikutana na Mahmoud Abbas mjini Ramallah Jumapili jioni, na walijadiliana juu ya sera za kiusalama, kiraia na masuala ya uchumi miongoni mwa masuala mengine.

Gantz alimwambia Abbas kuwa Israel inataka kuchukua hatuaza kuimarisha uchumi wa Palestina. Viongozi hao wawili walikubaliana kujadiliana zaidi juu ya masuala hayo.

Mkuu wa kitengo cha uratibu wa shughuli za serikali wa Israel Ghasan Alyan na mkuu wa idara ya Ujasusi wa Palestina Majid Faraj pia walishiriki kwenye mkutano huo.

Mkutano huo umefanyika muda mfupi tu baada ya Waziri Mkuu wa Israel Naftali Bennett kurejea kutoka nchini Marekani ambako alikutana na Rais Joe Biden na maafisa wakuu wa serikali ya Marekani.