Kiongozi wa kijeshi wa Sudan ziarani nchini Uganda
16 Septemba 2023Baraza la Utawala wa Sudan limesema, viongozi hao watajadili juu ya ushirikiano na masuala yenye umuhimu kwa mataifa hayo mawili.
Hiyo ni ziara ya sita ya al-Burhan tangu alipojitokeza hadharani mwezi uliopita baada ya kupotea machoni mwa umma katikati ya mapigano makali yaliyoshuhudiwa mjini Khartoum. Miongoni mwa mataifa ambayo tayari ameyatembelea ni pamoja na Misri, Sudan Kusini na Uturuki.
Sudan imekuwa katika machafuko tangu mapigano yalipoibuka mwezi Aprili kati ya jeshi rasmi linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al Burhan dhidi ya kikosi kilichoasi cha RSF chini ya aliyekuwa msaidizi wake Jenerali Mohamed Hamdan Daglo.
Kwa mujibu wa shirika linalofuatilia mizozo na kukusanya taarifa la "Armed Conflict Location & Event Data Project" takribani watu 7,500 wameuwawa tangu mgogoro ulipoibuka nchini humo Aprili 15.