1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Kiongozi wa kijeshi wa Sudan akutana na kiongozi wa Qatar

Sylvia Mwehozi
8 Septemba 2023

Kiongozi wa kijeshi wa Sudan Abdel Fattah al-Burhan amekutana na kiongozi wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani, wakati wa ziara yake ya tatu nje ya nchi tangu kulipozuka vita nchini mwake mnamo mwezi Aprili.

https://p.dw.com/p/4W5jQ
Qatar Doha | Sudan
Kiongozi wa kijeshi wa Sudan Abdel Fattah al-Burhan na kiongozi wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al ThaniPicha: Amiri Diwan/REUTERS

Kiongozi wa kijeshi wa Sudan Abdel Fattah al-Burhan amekutana na kiongozi wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani, wakati wa ziara yake ya tatu nje ya nchi tangu kulipozuka vita nchini mwake mnamo mwezi Aprili.

Burhan alikutana na kufanya mazungumzo na Sheikh Hamad Al Thani mjini Doha jana Alhamis na kugusia hali inayoendelea nchini Sudan na changamoto zinazoikabili nchi hiyo.

Kiongozi huyo wa Sudan pia amezitembea nchi za Misri na Sudan Kusinikatika siku za hivi karibuni. Vita nchini Sudan vimewaua watu takribani  5,000.

Siku ya Jumatano, Burhan alitoa amri ya kukivunja kikosi cha hasimu na makamu wake wa zamani Mohamed Hamdani Dagalo, cha RSF, wakati ambao pia Marekani ikitangaza vikwazo dhidi ya kamanda huyo.