1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis afanya ziara ya siku moja mjini Venice

Sylvia Mwehozi
28 Aprili 2024

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis anatembelea Venice, ikiwa ni ziara yake ya kwanza nje ya Roma ndani ya kipindi cha miezi 7, katikati mwa wasiwasi kuhusu afya ya kiongozi huyo aliye na umri wa miaka 87.

https://p.dw.com/p/4fGja
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis mjini VenicePicha: Alberto Pizzoli/AFP/Getty Images

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis anatembelea Venice, ikiwa ni ziara yake ya kwanza nje ya Roma ndani ya kipindi cha miezi 7, katikati mwa wasiwasi kuhusu afya ya kiongozi huyo aliye na umri wa miaka 87.

Papa Francis amefanya ziara nyingi duniani katika kipindi cha miaka 11 ya uongozi wake, lakini hajasifiri tangu alipozuru mji wa Ufaransa wa Marseille mnamo mwezi Septemba. Francis, ambaye anatumia kiti cha magurudumu, amepata matatizo ya kiafya katika miaka ya hivi karibuni, kutoka maumivu ya goti hadi upasuaji wa hernia na utumbo.

Kiongozi huyo alilazimika kusitisha ziara yake ya Dubai mwezi Desemba baada ya kuugua, ambako alitarajiwa kuhutubia hadhara ya Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya Tabianchi. Akiwa mjini Venice, Papa Francis atalitemebelea gereza la wanawake katika kisiwa cha Giudecca.