Papa Francis aongoza misa ya Pasaka
9 Aprili 2023Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis leo Jumapili ameongoza misa ya Pasaka katika uwanja wa kanisa la Mtakatifu Petro mjini Rome ambako maelfu ya Wakatoliki walikusanyika katika ibada hiyo. Misa ya Pasaka ilianza saa 10:00 asubuhi kwa saa za Ulaya ya kati ambapo baada ya misa baba Mtakatifu aliomba baraka za "Urbi et Orbi" - "Kwa miji na Ulimwengu" baada ya misa muda wa saa sita mchana. Papa hutumia kipindi hicho kutafakari matukio ya ulimwenguni. Katika Jumapili ya Pasaka, Wakristo husherehekea kufufka kwa Yesu Kristo na hivyo ushindi wa uzima juu ya kifo. Katika ujumbe wake kwenye usiku wa kuamkia Jumapili Papa Francis amelaani ukosefu wa haki uliokithiri na upepo wa vita, mambo ambayo amesema yametawala ulimwengu. Hata hivyo, kiongozi huyo wa kanisa katoliki amesema Pasaka huwatia watu moyo na kuwapa matumaini.