Kiongozi wa Iran afungua mlango wa mazungumzo ya Nyuklia
27 Agosti 2024Matangazo
Kiongozi mkuu mwenye mamlaka makubwa zaidi nchini Iran Ayatollah Ali Khamenei, amefungua mlango wa kukaribisha kuanzishwa tena mazungumzo na Marekani juu ya mpango wake wa Nyuklia.
Khamenei ameiambia serikali ya nchi yake kwamba hakuna kinachowazuia kufanya mazungumzo na adui. Kauli hiyo ya Khamenei inaonesha kufunguwa njia ya kukaribisha mazungumzo yoyote yatakayofanyika chini ya serikali inayoongozwa na rais mwanamageuzi Masoud Pezeshkian.
Hata hivyo Khamenei mwenye umri wa miaka 85, ambaye ana maamuzi ya mwisho kuhusu sera za Iran, amemtahadharisha Pezeshkian na serikali yake kutambuwa kwamba Marekani sio nchi ya kuaminiwa.