Haniyeh afanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Uturuki
21 Januari 2024Wanamgambo wa Hamas waliwachukua mateka zaidi ya watu 250 wakati walipoishambulia Israel Oktoba 7 na kuachiwa kwa mateka waliobakia pamoja na kusimamishwa kwa mapigano haraka iwezekanavyo, ndio mambo waliyoyajadili viongozi hao wawili walipokutana Uturuki.
Kulingana na duru za mkutano, Haniyeh na Fidan pia walijadili kuhusu kuongeza msaada wa kiutu mjini Gaza na pia suluhisho la kuwa na mataifa mawili kwaajili ya amani ya kudumu ya Israel na Palestina.
Kiongozi wa Hamas asema wako tayari kwa utawala mmoja wa Wapalestina
Israel imeapa kulisambaratisha kundi la Hamas kufuatia hatua yake ya kulishambulia Oktoba 7 na kusababisha mauaji ya waisraeli 1,140. Mashambulizi yanayoendelezwa na Israel katika ukanda wa Gaza hadi sasa yamesababisha mauaji ya wapalestina zaidi ya 24,000.