Kinywaji hiki ni maarufu na asili ya kabila la Wachaga linalopatika mkoani Kilimanjaro kaskazini mwa Tanzania. Mbege ni kinywaji kinachotengenezwa kwa mchanganyiko wa ndizi na ulezi na hupitia hatua kadhaa mpaka kufikia kuwa tayari kwa ajili ya matumizi.