Sudi Mnette amemkaribisha katika kiti cha mahojiano ya Kinagaubaga mwanasiasa wa siku nchini Tanzania James Mbatia. Hivi karibuni Mbatia ametumbukia kwenye mzozo na chama chake cha NCCR-Mageuzi ambacho kilitangaza kumfukuza ueneyekiti wa chama na uanachama. Mwenyewe anapinga madai yote yaliyosababisha kuchukuliwa hatua.