1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ni nani watakaonyakua nafasi 10 za mtoano Champions League?

27 Novemba 2023

Ligi ya vilabu bingwa barani Ulaya inasonga katika hatua za mwisho za mechi mbili za makundi kuanzia Jumanne ambapo matokeo yataathiri timu zitakazofuzu kwenye mashindano mengine ya kimataifa msimu huu na msimu ujao.

https://p.dw.com/p/4ZUc6
Ligi ya Vilabu Bingwa Ulaya, Bayern München - Galatasaray Istanbul
Mshambuliaji wa Bayern Munich Harry Kane akifunga goli dhidi ya GalatasarayPicha: Tom Weller/dpa/picture alliance

Kwa sasa timu ambazo tayari zishafuzu kwenye raundi ya mtoano ya 16 bora ni miamba wa Ujerumani Bayern Munich, mabingwa watetezi Manchester City, Real Madrid, Intermilan, RB Leipzig na Real Sociedad.

Zilizosalia ni nafasi 10 tu Napoli watasonga mbele iwapo watatoa ushindi watakapocheza na Real Madrid la sivyo watalazimika kusubiri mechi ya mwisho dhidi ya Braga mnamo Desemba 12.

Arsenal nao watafuzu iwapo watatoa sare watakapopambana na Lens uwanjani Emirates nao Atletico Madrid watapita iwapo watawalaza Feyenoord huko Uholanzi.

RB Leipzig - Manchester City
Wachezaji wa RB Leipzig Lois Openda na XaviPicha: motivio/ZB/picture alliance

Mambo bado hayajabainika yalivyo katika kundi F ambalo ndilo lililodaiwa kuwa kundi gumu zaidi. Borussia Dortmund, PSG, Newcastle na AC Milan timu yoyote inaweza kumaliza katika nafasi yoyote ile.

Hali ni ngumu vile vile katika kundi la Bayern Munich ambao washafuzu, ila Manchester United, Galatasaray na Copenhagen wote wanaweza kuchukua hiyo nafasi ya pili iliyosalia huku United wakielekea Istanbul Jumatano.

Vyanzo: AP/Reuters