1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kimbunga Saola chalipiga jimbo la Guangdong, China

2 Septemba 2023

Kimbunga Saola kimewasili katika jimbo la kusini mwa China la Guangdong leo alfajiri baada ya kufanya uharibifu kwenye miji ya Shenzhen, Hong Kong na Macau.

https://p.dw.com/p/4VsRz
Picha ya satelaiti ikionesha kimbunga Saola mjini Hong  Kong
Picha ya satelaiti ikionesha kimbunga Saola mjini Hong KongPicha: NASA WORLDVIEW/REUTERS

Kimbunga hicho kiliripotiwa kusababisha kifo cha mtu mmoja na mafuriko kwenye maeneo mengi.

Kikiambatana na upepo unaosafiri kwa kasi ya kilometa 200 kwa saa, kimbunga Saola kinatajwa kuwa ndiyo kikali zaidi kuwahi kulipiga jimbo la Guangdong tangu mwaka 1949.

Soma zaidi: Kimbunga Saola chaelekea miji mikubwa ya kusini mwa China

Wasiwasi wa kutokea madhara umezilazimisha mamlaka za jimbo hilo kufuta mamia ya safari za ndege, kuzifunga biashara, shule, na masoko pamoja na kuwahamisha zaidi ya watu 900,000.

Watabiri wa hali ya hewa wanasema kimbunga hicho sasa kinaelekea Taiwan na tayari mawimbi makubwa yameanza kushuhudiwa kwenye fukwe za kisiwa hicho.