1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kimbunga chauwa watu wanane Myanmar

22 Aprili 2023

Watu wanane wamekufa na wengine zaidi ya 200 wameachwa bila ya makazi baada ya vijiji viwili vya katikati mwa Myanmar.

https://p.dw.com/p/4QRQf
Indo-Myanmar-Grenze in Manipur und Mizoram
Picha: Mani Tewari Prabhakar/DW

Watu wanane wamekufa na wengine zaidi ya 200 wameachwa bila ya makazi baada ya vijiji viwili vya katikati mwa Myanmar, karibu na mji mkuu wa Naypyitaw kukumbwa na kimbunga.Shirikia la kutoa misaada-Thet Paing Soe, limevitaja vijiji ambavyo vimekumbwa na kadhia hiyo kuwa ni Aung Myin Kone na Tadau. Taarifa yao inasema majeruhi 128 walipelekwa hospitali huku nyumba 232 zikiporomoka kabisa.Katika kipindi cha mvua nyingi nchini Myanmar kumekuwa na hali ya kutokea majanga yatokanayo na hali ya hewa karibu kila mwaka. Ikumbukwe tu, 2008, Kimbunga Nargis kiliua zaidi ya watu 138,000.