1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMadagascar

Kimbunga cha kitropiki kimesababisha mafuriko na maporomoko

30 Januari 2023

Kimbunga cha kitropiki kimesababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi katika maeneo mbali mbali ya Madagascar na kusababisha vifo vya watu 30 na wengine 20 hawajulikani waliko.

https://p.dw.com/p/4Mt2z
DW 2022 - Ein Jahr mit extremen Wetterereignissen in Afrika
Picha: DW

Maelfu ya watu wameathirika kufuatia kimbunga hicho kilichopiga Kaskazini Mashariki mwa kisiwa hicho alhamisi iliyopita.

Ripoti ya awali kuhusu kimbunga Cheneso, iliyotolewa na ofisi ya taifa inayosimamia majanga, imeeleza kwamba takriban watu 89,000 wameathiriwa na janga hilo na majumba kadhaa yameporomoka na kuna watu walionasa kwenye maporomoko ya ardhi.

Soma pia:Zaidi ya watu 30,000 waathiriwa na kimbunga Madagascar

Watu wapatao 33,000 wamelazimika kuondoka kwenye makaazi yao katika mkoa wa Boeny kaskazini Mashariki mwa Madagascar.