SiasaAsia
Kim Jong Un akutana na ujumbe wa China
27 Julai 2023Matangazo
Shirika la habari la Korea Kaskazini limeeleza kuwa Kim leo amemkaribisha Li Haongzhong mjini Pyongyang, ambapo alimkabidhi barua rasmi ya Rais wa China, Xi Jinping.
Kim amekutana pia Waziri wa Ulinzi wa Urusi, Sergei Shoigu, ambapo walikuwa na mazungumzo ya kirafiki.
Soma zaidi: Korea Kaskazini yarusha makombora mawili, baada ya nyambizi ya Marekani kuwasili Korea Kusini
Shoigu alimkabidhi pia Kim barua iliyoandikwa na Rais wa Urusi, Vladmir Putin.
Urusi, mshirika wa kihistoria wa Korea Kaskazini, ni mojawapo ya mataifa machache ambayo Pyongyang imedumisha uhusiano wa kirafiki.
Korea Kaskazini leo inaadhimisha miaka 70 ya makubaliano ya kusitisha mapigano ya mwaka 1953, ambayo yalimaliza uhasama kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini.