Kila jamii ina mtazamo wake kuhusu bangi
Watu wanaopinga bangi wanaichafulia sifa, na wanaoikubali wanaiona kuwa ni mwarobaini wa kila kitu duniani. Kwa miongo kadhaa, mengi yamezungumzwa juu ya bangi kuliko mmea mwingine wowote.
Mmea wa imani isiyo kweli
Bangi ni miongoni mwa mihadarati. Kuna tofauti za mimea ya bangi ndio sababu Ujerumani inadhibiti kilimo cha mmea huo. Tofauti na miaka 200 iliyopita, mmea huo haufuatiliwa sana na watu nchini Ujerumani ndio sababu kuna taarifa zisizo sahihi zinaenezwa na makundi yanayoikubali bangi na yanayoipinga.
Wanajeshi wa Ufaransa wapeleka dawa ya kulevya aina ya hashish nchini mwao
Utumiaji wa bangi kama kileo una historia ya kulinganishwa ya hivi karibuni barani Ulaya. Wanajeshi wa Ufaransa ambao walichukua dawa ya kulevya ya hashish iliyotengenezwa kutoka kwa mimea ya kike ya bangi katika kampeni ya Napoleon ya Misri mnamo 1798, walitekeleza jukumu kubwa katika kuieneza. Wakati Napoleon alipopiga marufuku ya hashish nchini Misri, ikaibuka kuwa maarufu huko Paris.
Bangi yatumika kama tiba ya maumivu ya hedhi
Tangu miaka ya 1990, Uingereza imekuwa ikijadili kuhusu kuhalalishwa kwa bangi. Kulikuwa na uvumi wakati huo kwamba Malkia Victoria alitakiwa kutumia bangi kwa maumivu ya hedhi. Ushahidi pekee ni wa mwaka 1890, wakati daktari wake wa kibinafsi John Russel Reynolds aliandika katika jarida la matibabu "thamani kubwa" ya bangi katika kutibu magonjwa mbali mbali
Ngozi au bangi?
Usemi ulioko mijini ni kwamba Azimio la Uhuru wa Marekani liliandikwa kwenye karatasi iliyotengenezwa kutokana na bangi. lakini hiyo si kweli kabisa. Hati hiyo, iliyoko katika hifadhi ya kitaifa huko Washington, DC, iliandikwa kwenye karatasi ya ngozi. Rasimu mbili za kwanza, kwa upande mwingine, labda ziliandikwa kwenye karatasi ya bangi
Filamu ya Reefer Madness
"Reefer Madness," filamu iliyofadhiliwa awali na kikundi cha kanisa chini ya kichwa cha "Mwambie Mtoto Wako," ilikuwa filamu ya propaganda ya Marekani ya mwaka wa 1936 ambayo ilionyesha vijana kama waraibu, wenye vurugu na wazimu, mara tu baada ya kuvuta bangi. Pamoja na kutilia chumvi zaidi vichekesho na imani potofu, filamu hiyo ni ushuhuda wa kihistoria wa kuchochea hofu katika enzi hizo.
Maneno ya ubaguzi wa rangi
Wakati huo, Harry Anslinger, mkuu wa shirika la kukabiliana na dawa za kulevya nchini Marekani, alikuwa akipigania kupigwa marufuku kwa matumizi ya bangi. Inadaiwa kuwa, raia wa Mexico na Wamarekani weusi ndio waliotumia zaidi bangi, lakini Anslinger hakuwa na wasiwasi kuhusu afya zao. Anslinger aliwahi kusema kuwa bangi, huwafanya watu weusi wafikirie kuwa wao ni bora kama wazungu.
Ibada ya kidini
Tamaduni zingine labda ziko wazi zaidi juu ya athari za bangi. Maandishi matakatifu kuhusu mungu wa Kihindu Shiva yanasema kwamba aliachana na anasa zote za maisha isipokuwa bangi. Kinyume na madai yanayorudiwa mara kwa mara, matumizi ya bangi yanaweza kusababisha uraibu.