Kikosi cha Ulaya Ukanda wa Sahel chatakiwa kuondoka Niger
1 Machi 2024Matangazo
Msemaji wa Umoja wa Ulaya aliliambia hayo shirika la habari la Ujerumani (dpa) mjini Brussels kwamba Umoja huo umelazimishwa kuharakisha mchakato wa kukiondoa kikosi cha EUCAP.
Soma zaidi: Jumuiya ya ECOWAS yaiondolea Niger baadhi ya vikwazo
Mnamo mwezi Disemba, utawala wa kijeshi wa Niger uliamua kufuta ushirikiano na makundi mawili ya Umoja wa Ulaya, likiwemo hilo la EUCAP Sahel Niger na EUMPH, ambalo ni la ushirikiano wa kijeshi.
Wiki iliyopita, Umoja wa Ulaya ulilaani vikali shambulizi dhidi ya makao makuu ya kikosi cha EUCAP mjini Niamey, ambapo vifaa vya kikosi hicho viliporwa.
Kikosi hicho chenye takribani wanajeshi 130 kilikusudiwa kusaida katika vita dhidi ya ugaidi katika Ukanda wa Sahel.