Kikosi cha MONUSCO chaondoka rasmi Kivu Kusini
25 Juni 2024Hafla yakuondoka imefanyika katika Kijiji cha Kavumu kwenye umbali wa kilomita 33 kaskazini mwa mji wa Bukavu ambako ameshiriki pia waziri Mkuu wa Congo Judith Suminwa Tuluka.
Katika hafla hiyo Mkuu wa Tume ya Amani ya Umoja wa Mataifa Nchini Congo Monusco Bintou Keita ameishukuru serikali ya Kongo kwa ushirika wake katika kufanikisha amani lakini pia kusisitiza kwa mara nyingine kwamba baada ua Monusco kuondoka, Serikali ya Congo inabaki na wajibu mkubwa kulinda raia wake.
Kivu Kusini inakabiliwa na kitisho baada ya jeshi la Umoja wa Mataifa kuondoka
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani , Naibu Waziri Mkuu anayeshughulikia Mambo ya Ndani Jacquemin Shabani alikiri kuwa hali ya usalama bado ni tete na kuahidi kuwa juhudi zitafanyika kuhakikisha usalama katika jimbo zima la Kivu Kusini. Jacquemin Shabani anaeleza.
MUNUSCO imekuwa katika operesheni ya moja kwa moja ya ardhini nchini Kongo tangu mwaka 2002, ikiwa na wajibu mkubwa wa kulisadia jeshi la taifa hilo katika wajibu wa kuwalinda watu wake. Baada ya Kivu Kusini, MONUSCO inakusudia kuendelea na mchakato wa kujiondoa katika majimbo ya Kivu Kaskazini, na Ituri.