1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Khamenei amuidhinisha rasmi Pezeshkian kuwa rais wa Iran

28 Julai 2024

Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei amemuidhinisha rasmi mwanamageuzi Masoud Pezeshkian kama rais wa tisa wa nchi hiyo kufuatia uchaguzi wa haraka uliokamilika mapema. mwezi huu.

https://p.dw.com/p/4ipmW
Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei( kushoto) na Rais mteule wa Iran Masoud Pezeshkian (kulia) wakati wa hafla ya kuidhinishwa rasmi kwa Rais huyo mteule
Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei( kushoto) na Rais mteule wa Iran Masoud Pezeshkian (kulia)Picha: leader.ir

Katika ujumbe uliosomwa na mkurugenzi wa ofisi ya Khamenei, kiongozi huyo amesema kuwa anamuidhinisha Pezeshkian aliyemtaja kama mtu mwenye hekima, mwaminifu, maarufu na msomi na kwamba anamteuwa kuwa rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Rais huyo mpya anatarajiwa kuapishwa mbele ya bunge siku ya Jumanne.

Soma pia:Masoud Pezeshkian: Nini cha kutarajia kutoka kwa rais mpya wa Iran

Sherehe za uidhinishaji huo zilifanyika katika mji mkuu Tehran na kuhudhuriwa na maafisa wakuu wa Iran pamoja na wanadiplomasia wa kigeni, na kupeperushwa kupitia televisheni ya serikali.

Pezeshkianalishinda duru ya pili ya uchaguzi wa rais mnamo Julai 5 dhidi ya mhafidhina Saeed Jalili, kuchukuwa nafasi ya rais Ebrahim Raisi aliyefariki katika ajali ya helikopta mwezi Mei.