Kesi ya kiongozi wa zamani wa Liberia Charles Taylor yaanza kusikilizwa
5 Juni 2007Matangazo
Charles Taylor anatuhumiwa kulifadhili kundi la waasi katili la Revolutionary United Front RUF lililoendesha vita vya kikatili vya miaka 11 vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sierra Leone vilivyoua maelfu ya watu.
Hata hivyo Charles Taylor mwenyewe hakufika mahakamani, na wakili wake Karim Khan aliondoka mahakamani kufuatia majibishano na jaji akisema mteja wake anaona hatatendewa haki kwa kuwa na wakili mmoja.
Aboubakary Liongo amezungumza na mkuu wa Idara ya Habari katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya mjini Freetown,Sierra Leone alikoshtakiwa mara ya kwanza Charles Taylor, Said Msonda. Kwanza alitaka kujua wananchi wa huko wanaifuatilia vipi kesi hiyo.