1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya kuchukua hatua kali dhidi ya dawa za kututumua misuli

24 Novemba 2022

Wizara ya michezo nchini Kenya imesema "inachukua hatua madhubuti" kuzuia uwezekano wa kupigwa marufuku kwa wanariadha wake kimataifa kufuatia msururu wa visa vya matumizi ya dawa za kutunisha misuli.

https://p.dw.com/p/4K0LO
2015 Ezekiel Kemboi und andere kenianische Läufer überqueren die Ziellinie
Picha: Getty Images/P. Smith

Zaidi ya wanariadha 30 wa Kenya wamesimamishwa au kupigwa marufuku kwa makosa ya kutumia dawa za kutunisha misuli mwaka huu.

Hali tete ya nchi hiyo inatarajiwa kuwa ajenda kuu wakati wa mkutano kati ya wakala wa Kupambana na Dawa za Kulevya Duniani (WADA) na Kitengo cha Uadilifu wa Riadha (AIU) mjini Monaco Ijumaa.

Waziri wa Michezo Ababu Namwamba amesema serikali inatumia mbinu zote zilizopo ili kukabiliana na tatizo hilo na kuepuka aibu hiyo.