1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Katibu mkuu wa NATO kubakia madarakani kwa mwaka mwingine

5 Julai 2023

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami NATO Jens Stoltenberg atabakia katika nafasi hiyo kwa mwaka mwingine akisema muungano huo wa kijeshi ni muhimu zaidi kuliko wakati mwingine wowote katika dunia ya sasa iliyo hatari.

https://p.dw.com/p/4TQrQ
Jens Stoltenberg, NATO
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami NATO Jens StoltenbergPicha: Heiko Becker/REUTERS

Stoltenberg amesema jana kuwa ameurefusha mkataba wake kwa miezi 12. Mnorway huyo amesema ni fahari kwake kubakia katika wadhifa huo kwa mwaka mwingine, akisema muungano huo wa kijeshi ni muhimu zaidi kuliko wakati mwingine wowote katika dunia ya sasa iliyo hatari. Awali, alitarajiwa kuwachia ngazi mwaka huu. Lakini nchi za NATO zimepatwa na changamoto ya kumpata mrithi wa Stoltenberg katika wakati huu mgumu wa jumuiya hiyo kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine. Wagombea kadhaa wa kumrithi Mnorway huyo ambaye ni waziri mkuu wa zamani walijitokeza na kisha kujiondoa kinyang'anyironi katika miezi ya karibuni.